1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Mzozo wa gesi kati ya Gsprom na Belarus waendelea

31 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCeo

Kuna taarifa za kutatanisha juu ya makubaliano kati ya kampuni pekee ya gesi nchini Urussi Gazprom na serikali ya Belarus yenye lengo la kuutatua mzozo wa kiwango cha bei ya gesi inayotozwa Belarus na kampuni hiyo ya Urussi.

Maafisa wa Belarus wanasema makubaliano juu ya suala hilo yamefikiwa lakini wawakilishi wa Gazprom wamekanusha juu ya kufikiwa makubaliano yoyote na kusema kwamba bado mazungumzo yanaendelea.

Kampuni ya gesi ya Gazprom imetishia kukata huduma ya gesi kwa Belarus mwanzoni mwa mwaka mpya hadi pale serikali ya mjini Minsk itakapokubali kulipa mara mbili zaidi ya kiwango inacholipa sasa.

Rais wa Belarus Alexander Lukashenko amesema nchi yake haiwezi kudhalilishwa na kile alichokitaja kuwa vitisho.