1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW.Mzozo wa maafisa wa jeshi la Urusi waendelea baina ya nchi hiyo na Georgia

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6n

Vyombo vya habari nchini Urusi vimeripoti juu ya amri iliyotolewa na serikali ya kukatiza mawasiliano yote ya usafiri baina ya nchi hiyo Georgia.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Georgia kutamka kuwa itawakabidhi maafisa wanne wa kijeshi wa Urusi kwa shirika linalo husika na maswala ya usalama.

Maafisa hao wanne ndio chanzo cha mzozo uliopo baina ya nchi hizo mbili.

Maafisa hao walikamatwa wiki iliyopita na kukabiliwa na makosa ya ujasusi jambo ambalo lilisababisha Urusi kuwaondoa baadhi ya maafisa wake wa kidiplomasia kutoka mji wa Tbilisi nchini Georgia.

Rais Vladmir Puttin wa Urusi ametaja kukamatwa kwa mafisa hao kuwa ni sawa na ugaidi baina ya mataifa kama uliotokea mwaka 1930 na ambao ulisababisha kuuwawa takriban raia milioni moja kutoka Usovieti.