1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Putin kushikilia msimamo mkali kabla mkutanmo wa G8

4 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuq

Rais wa Urusi Vladimir Putin anashikilia msimamo wake mkali kuhusu masuala ya makombora ya kulipiza kisasi na kutetea kuuliwa kwa afisa wa zamani wa ujasusi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin anaionya Marekani kuwa mpango wa kuweka makombora ya kujihami katika eneo la Ulaya Mashariki huenda kukasababisha wao kurusha makombora ya kulipiza kisasi.

Marekani inapanga kuweka makombora hayo ya kujihami nchini Poland.Viongozi wenzake katika kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda ulimwenguni G8 wanaokutana mjini Heiligendamm hapa Ujerumani wanatilia shaka msimamo mkali wa Urusi.Mkutano huo wa kilele unapangwa kufanyika kuanzia tarehe 6-9 mwezi huu.