1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Rais Putin ashikilia hakuna mvutano ila tofauti

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1c

Rais wa Urusi Vladimir Putin anashikiia kwamba hakuna mvutano wowote kati ya Urusi na Umoja wa Ulaya ila mitizamo tofauti kuhusu masuala yanayohitaji suluhu.Urusi na Umoja wa Ulaya unapanga kufanya mkutano mjini Samara nchini Urusi mwishoni mwa juma.Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier aliyekutana na Rais Putin hatua imepigwa. Pande hizo mbili zimekuwa na tofauti kuhusu masuala kadhaa likiwemo vikwazo ilivyowekewa nchi ya Poland vya biashara ya nyama .Nchi ya Poland ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na inasema kuwa itapiga kura ya turufu endapo majadiliano mapya yataanzishwa katika ya Umoja huo na Urusi.

Wakati huohuo Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bi Condoleeza Rice na Rais wa Urusi Vladimir Putin wanakubaliana kubadili kauli zao ili kuimarisha uhusiano kati yao.Hata hivyo kulingana na Bi Rice aliyefanya mkutano na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov,Urusi inapinga mpango wa Marekani wa kuunda kituo cha makombora ya kujilinda katika nchi za Poland na Jamhuri ya Czech.Urusi aidha inapinga mpango wa Umoja wa Mataifa unaoungwa mkono na Marekani kuruhusu jimbo la Kosovo la Serbia kupata uhuru japo kwa kusimamiwa.