1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Urusi yaanza tena kupitisha mafuta Belorussia

11 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCbt

Urusi imeanza tena kupitisha mafuta kwenda katika nchi za Ulaya ya magharibi katika bomba linalopitia Belorussia.

Umoja wa Ulaya umeelezea kufurahishwa kwake na hatua hiyo ya muafaka iliyofikiwa kati ya Urusi na Belorussia.

Hapo siku ya Jumapili Urusi ilisitisha kupitisha mafuta yake katika bomba linalopita Belorussia ikidai kuwa nchi hiyo ilikuwa ikifyonza mafuta yake.Belorussia ilikuwa ikidai Urusi ilipe dola 45 kwa kila tani ya mafuta kama kodi kwa bomba hilo kupitia katika ardhi yake.

Mapema kamishna wa ulaya anayehusika na nishati Andris Piebalgs aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kuwa hakukupatikana utatuzi wa moja kwa moja juu ya mzozo huo kwenye mazungumzo kati yao na balozi wa Urusi katika umoja wa Ulaya.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya umeelezea mapendekezo kuelekea katika uanzishwaji wa utaratibu wa kufuatwa katika matumizi ya nishati.

Rais wa kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barroso amesema kuwa mipango hiyo itauweka Umoja wa Ulaya mstari wa mbele katika juhudi za kupambana na mabadiliko ya hali hewa duniani.