1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Urusi yakataa jasusi wake kupelekwa Uingereza

23 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzK

Urusi imelikataa ombi la Uingereza la kutaka kumkabidhi jasusi wa zamani wa nchi hiyo, ili akashtakiwe kuhusiana na kifo cha jasusi mwenzake wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko mwaka jana.

Urusi imesema kufanya hivyo ni kinyume na katiba ya nchi hiyo inayopinga raia wa nchi hiyo kwenda kushtakiwa katika nchi nyingine.

Uingereza inamshuku Andrei Lugovoi kuwa alimpa sumu Litvinenko kwa njia ya miale Novemba mwaka jana, baada ya kukutana kwenye mgahawa mmoja mjini London pamoja na mfanyabiashara wa kirusi.

Litvinenko alianza kuumwa muda mfupi tu baada ya kumaliza kukutana na jasusi huyo mwenzake wa zamani, na wiki tatu baadaye akafariki.

Lugovoi amekanusha madai hayo ya kumuua Litvinenko ambaye alikimbilia uhamishoni Uingereza.