1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Urussi yaitaka Marekani kukoma na mpango wa makombora ya ulinzi

10 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBt6

Waziri wa mambo ya nje wa Urussi Sergei Lavrov ameitaka Marekani kusimamisha mazungumzo yake kuhusu makombora ya ulinzi na jamhuri ya Czech na Poland hadi watakapojadiliana juu ya suala hilo.

Matamshi hayo yamekuja siku moja baada ya rais Bush kukutana na mwenzake wa Poland Lech Kachinski na kuashia kwamba mipango ya kuweka makombora ya ulinzi itaendelea.

Mpango huo wa Marekani umezusha mvutano mkubwa kati ya serikali ya mjini Washington na Moscow katika kipindi cha miezi kadhaa sasa.

Wakati huo huo mamia ya waandamanaji wameandamana hadi kwenye uwanja wa St Petersberg kupinga sera za rais Vladmir Putin wa Urusi.Maandamano hayo ni mfululizo wa maandamano kadhaa ya wafuasi wa upinzani ambao wanamshutumu Putin kwa kurudisha nyuma maendeleo ya demokrasia kabla ya kufanyika uchaguzi war ais nchini humo hapo mwakani.