1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSKOW.Kiongozi wa Hamas yuko nchini Urusi kwa mazungumzo na rais Puttin

26 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOK

Kiongozi wa chama cha Hamas kinacho tawala maeneo ya Palestina amewasili mjini Moskow, Urusi kwa mazungumzo na rais Vladmir Puttin.

Viongozi hao watalipa umuhimu swala la kuunda serikali ya umoja kati ya vyama vya Hamas na Fatah katika mazungumzo yao.

Ziara hiyo ni ya pili kufanywa na kiongozi huyo wa Hamas mjini Moskow tangu chama chake kishinde katika uchaguzi wa Januari mwaka uliopita.

Kundi la Hamas linajitahidi kutafuta uungwaji mkono na kumaliza vikwazo vya kiuchumi vilivyo wekwa na pande nne zinazoshughulikia mgogoro wa mashariki ya kati.

Wakati huo huo mji wa Nablus ulio kati kati ya Ukingo wa magharibi bado uko chini sheria za kutotoka nje kwa siku ya pili mfululizo huku Israel ikiendelea na msako ambao imeutaja kuwa ni wa kuwasaka magaidi.

Kwa mujibu wa walioshuhudia ni kwamba takriban magari 60 ya kijeshi ya vifaru yaliingia katika mji wa Nablus jana na kutangaza sheria hiyo ya kutotoka nje.

Jeshi la Israel limesema kuwa huenda msako huo ukachukua siku kadhaa, takriban wapalestina 20 walikamatwa na kumi na tano kati ya hao wakaachiliwa baada ya muda mfupi. Palestina imelaani hatua hiyo na imesema, itatatiza makubaliano ya amani.