1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSKOW.Urusi kusitisha ujenzi katika kinu cha nyuklia cha Iran

19 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQh

Urusi imesema kuwa itasitisha ujenzi katika kinu cha Bushehr nchini Iran kwa sababu Tehran imechelewesha malipo ya mradi huo.

Kwa mujibu wa duru za shirika la nishati ya nyuklia la Rosatom, Urusi ilianzisha shughuli za ujenzi wa kinu cha kwanza cha nyuklia cha Iran tangu mapema miaka ya 90.

Urusi imekuwa ikisitisha ujenzi huo mara kwa mara kwa sababu za kiufundi licha ya Iran kukabiliwa na shinikizo kutoka nchi za magharibi zinazoitaka nchi hiyo kuacha mapango wake wa nyuklia.

Moskow ilitarajiwa kuanza kupeleka nishati ya nyuklia katika kinu hicho kuanzia mwezi Machi ili kukitayarisha kinu hicho kilichopangiwa kuanza kazi yake rasmi mwezi Septemba.

Urusi na Iran hata hivyo zinasema kuwa kinu hicho kitazalisha nishati ya umeme pekee na wala sio vinginevyo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limependekeza vikwazo dhidi ya Iran baada ya nchi hiyo kushindwa kuacha mpango wake wa kuzalisha madini ya Uranium.