1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto katika Mlima Kenya

18 Januari 2012

Nchini Kenya moto katika mlima Kenya unaendelea kuwaka kwa siku ya nne sasa. Moto katika mlima huo ulio na urefu wa mita zaidi ya Elfu 4 na wa pili kwa ukubwa barani Afrika ulianza Jumamosi usiku.

https://p.dw.com/p/13lG8

Sasa wakaazi katika eneo hilo wanasema wana hofu kuwa huenda wanyamapori katika eneo hilo wakaanza kuingia katika makaazi yao huku wengine wakiilaumu serikali kwa kushindwa kuudhibiti moto huo. Mlima Kenya unachangia asilimia 80 ya uzalishaji wa umeme unaotokana na vyanzo vya maji.

Amina Abubakar amezungumza na Mkurugenzi wa shirika la huduma za wanyama pori nchini Kenya, KWS,Julius Kipngetich kujua hali kwa sasa hivi iko vipi.

Mwandishi: Amina Abubakar

Mhariri: Mohammed Khelef