1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moyes asema Man United itapigana hadi mwisho

20 Januari 2014

Kocha wa Manchester United David Moyes ameahidi kutosalimu amri licha ya timu yake kubakia nyuma zaidi ya viongozi wa ligi na pengo la pointi 14 baada ya kushindwa na Chelsea.

https://p.dw.com/p/1Atuj
FC Everton Trainer David Moyes
Picha: Getty Images

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amedokeza kuwa matumaini ya United kutetea taji la Ligi Kuu ya Soka ni kama yamekwisha kabisa baada ya Samuel Eto'o kutikisa wavu mara tatu katika ushindi wa Chelsea wa magoli matatu kwamoja. Moyes hata hivyo amesema vijana wake bado watapigana hadi mwisho.

Amesema kazi yao ni kujaribu wawezalo ili kumaliza katika nafasi ya kwanza. Kinyang'anyiro kinaonekana kuwa kikali, wakati Arsenal wakiongoza na pointi 51 baada ya kuwafunga Fulham magoli mawili kwa sifuri, wakati nao Manchester City wakiwa wa pili na pointi 50. Chelsea ni wa tatu na pointi 49.

La liga yapamba moto

Nchini Uhispania, Real Madrid imejiweka katika nafasi nzuri kabisa ya kuwania taji la msimu huu la La Liga, baada ya viongozi wa ligi Barceolona na Atletico Madrid kutekwa sare katika mechi zao.

Barca waikabwa na Levante kwa kufungana goli moja kwa moja wakati Atletico Madrid wakifungana goli moja kwa moja na Sevilla. Baraca na Atletico wana pointi 51 wakati Real wakiwa na pointi 50 kufiatia ushindi wao wa mabao matano kwa sifuri dhidi ya Real Betis siku ya Jumamosi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman