1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kufufua uchumi wa Marekani

Oumilkher Hamidou24 Januari 2009

Warepublöican wataka mpango wa kufufua uchumi wa Marekani ufanyiwe marekebisho

https://p.dw.com/p/GfLd

Washington:


Rais mpya wa Marekani Barack Obama amewatolea mwito wa dhati wafuasi wa upande wa upinzani wa Republican,waunge mkono mpango wake wa kutengwa dala bilioni 825 kwaajili ya kuinua ukuaji wa kiuchumi."Marekani inakabwa na mzozo wa kiuchumi usiokua na mfano,na hatua za haraka zinahitajika " amesema hayo rais Obama alipokutana na wawakilishi wa ngazi ya juu wa baraza la Congress katika ikulu ya White House.Warepublican wanadai mpango huo ambao rais Obama anapanga kuufikisha mbele ya baraza la Congress kati kati ya mwezi ujao wa february,ufanyiwe marekebisho ya kina.Mkuu wa upande wa upinzani katika baraza la wawakilishi la Marekani John Boehner amesisitiza akisema tunanukuu"Ili kuweza kuinua uchumi kodi za mapato zinabidi zipunguzwe na  itolewe misaada kwa wanaotaka kununua nyumba"Mwisho wa kumnukuu mkuu wa upande wa upinzani katika baraza la wawakilishi anaehisi mpango wa rais Obama wa kufufua uchumi unagharimu fedha nyingi.