1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpatanishi Jalili wa Iran kukutana na Solana

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQPh

Mpatanishi mkuu wa Iran kuhusika na mradi wa nyuklia wa nchi hiyo,Saeed Jalili amesema atakutana na mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya Javier Solana tarehe 30 Novemba.Hiyo itakuwa juhudi mpya ya pande hizo mbili kuendelea na majadiliano yaliyokwama kuhusika na mradi wa nyuklia wa Iran.Nchi za Magharibi zina hofu kuwa mradi huo una azma ya kutengeneza silaha za kinyuklia kwa siri.Solana,mwishoni mwa mwezi huu wa Novemba anatazamiwa kutoa ripoti yake mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,kueleza kwa umbali gani Iran ipo tayari kusitisha harakati za kurutubisha madini ya uranium.Ripoti ya Solana itasaidia kuamua iwapo Iran iwekewe vikwazo vipya.Iran inashikilia kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya kiraia tu.