1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

130709 Nabucco Pipeline Ankara

Abdu Said Mtullya13 Julai 2009

Mradi wa Nabucco kuanza kutekelezwa .Lengo ni kupunguza kuitegemea Urusi kwa mahitaji ya gesi.

https://p.dw.com/p/IoWx
Picha: AP

Katika  juhudi  za kuepuka matatizo ya ugavi  wa gesi kutoka Urusi,  nchi  nne za  Umoja  wa Ulaya  pamoja  na Uturuki zimetiliana  saini  makubaliano  juu  ya ujenzi  wa  bomba  la  gesi kutokea bahari   ya  Caspian .

 Mradi huo unatazamiwa kumalizika mnamo  mwaka  2014. Lakini pana maswali ya kuuliza.

Jee Fedha  zitatoka wapi, ili kuutekeleza na gesi yenyewe  itatoka  wapi ?

Uturuki na nchi  nne  za Umoja  wa Ulaya leo zimetiliana  saini leo makubaliano  juu kutelekeza mradi wenye lengo  la kuziwezesha nchi za Ulaya  kupunguza kuitegemea Urusi kwa  mahitaji yao  ya gesi. Mradi huo ni wa kujenga  bomba  la gesi litakalopitia katika nchi hizo  tano  kutokea   bahari ya  Caspian kwa  kuikwepa Urusi.

Nchi hizo ni Austria, Hungary, Romania,Bulgaria na Uturuki.

Waziri  mkuu  wa Uturuki  Erdogan amesema leo kwenye  sherehe  ya kutiliana saini mjini  Ankara , kwamba msingi  wa  kuanza  kujenga  bomba hilo  umeshawekwa.Bomba hilo la  gesi litakalokuwa na  urefu  wa  kilometa 3300  linatazamiwa kukamilika mnamo mwaka 2014. Gesi  kiasi  cha  kubik meta bilioni  31 kitapitia katika bomba hilo litakalopitia  katika nchi hizo tano.Mazungumzo juu ya mradi wa bomba hilo  unaoitwa Nabucco yalianza kufanyika  mwaka 2002.

Waziri Mkuu  wa  Bulgaria Sergei Stanichew alietia saini mkataba wa mradi wa Nabucco kwa niaba  ya nchi yake amesema nchi zao bado ziko mbali kukamilisha mradi  wa  Nabucco kwa miaka kadhaa  lakini kwa  serikali ya Bulgaria  na kwa watu wa  nchi yake waliokabiliwa na hali mbaya sana wakati wa mgogoro wa nishati katika mwezi januari,  hatua ya  kutiwa saini mkataba huuleo, ni ujumbe  madhubuti kisiasa  na kiuchumi.

Hatahivyo  bado pana maswali yanayopaswa kujibiwa juu  ya  mradi  wa Nabucco;  kwa mfano gesi inayokusudiwa  kuletwa  barani  Ulaya kwa kupitia  katika  nchizilizotia saini leo itatoka  wapi? Mpaka  sasa  ni Azerbaijan  tu inayoonekana    kuwa mgavi imara wa gesi hiyo.

Swali jingine linahusu  fedha za kugharamia  mradi huo wa Euro bilioni nane.Umoja wa Ulaya hadi sasa umeahidi   Euro milioni 250 tu.

Mwandishi/Kilian Pfeffer.

Mfasiri Mtullya. A.

ZA.