1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wa mgodi wauwa 40 nchini China

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYG7

BEIJING

Mripuko wa gesi katika mgodi wa makaa ya mawe kaskazini mwa China umeuwa takriban watu 40 wakati nwengine 74 wakiwa bado hawajulikani walipo.

Televisheni ya taifa nchini China imeripoti kwamba wafanyakazi wa migodi 13 wameokolewa baada ya kutokea kwa mripuko huo ndani ya mgodi kwenye mji wa Linfen katika jimbo la Shanxi lakini haikutowa maelezo zaidi.

China imekuwa ikijaribu kuimarisha taratibu za usalamu kwenye migodi yake lakini bado migodi ya nchi hiyo inaendelea kuwa mibaya kabisa duniani kwa kugharimu maisha ya karibu watu 5,000 mwaka jana.

Wamiliki wa migodi wanalaumiwa kwa ajali nyingi zinazotokea kwa kupuuza sheria za usalama na kushindwa kuwekeza katika zana za kuingiza hewa kwenye migodi, kudhibiti moto na zana nyenginezo.