1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msafara wa magari ya kijeshi ya Libya wawasili Niger

6 Septemba 2011

Inakisiwa huenda kanali Gaddafi yumo njiani kwenda Burkina Fasso, ambayo ilikuwa imesema ingemkubali kiongozi huyo kwenda uhamishoni nchini humo.

https://p.dw.com/p/12Tel
Aliyekuwa kiongozi wa Libya, Muammar GaddafiPicha: dapd

Msafara mkubwa wa magari ya kivita ya Libya uliosindikizwa na wanajeshi wa Nigeria umewasili katika mji wa Agadez ulioko eneo la jangwani, kaskazini mwa Niger. Kwa mujibu wa duru za kijeshi za Ufaransa na Niger, msafara huo uliwasili jana jioni.

Msafara huo ni wa kiasi ya magari 250 ya jeshi la Libya uliowaleta maafisa wa vikosi vya eneo la kusini na huenda safari yao ilianzia Algeria kabla ya kuwasili Niger. Kwa mujibu wa duru za kijeshi za Ufaransa, Kanali Muammar Gaddafi na mwanawe wa kiume Saif al Islam huenda wakajiunga na msafara huo unaoripotiwa kuelekea Burkina Faso.

Ifahamike kuwa serikali ya nchi hiyo ya Afrika Magharibi inayopakana na Niger imeahidi kumhifadhi Kanali Gaddafi na familia yake.