1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshindi wa mita 800 ni mwanamke ?

20 Agosti 2009

Ulimwengu wa riadha wauliza Berln ?

https://p.dw.com/p/JEhh
Robert HartingPicha: AP

Ujerumani ilijipatia medali yake ya pilii ya dhahabu jana usiku katika mashindano ya riiadha ulmwengun mjiini Berlin.Kenya ilitoka mikono mitupu katika finalii ya mita 1500-dhahabu na shaba ziliwaendea wazaliwa wa Kenya wanaokimbia chini ya bendera ya Bahrein na Marekani: Yusuf Kamel na Bernard Lagat.

Macho ya mashabiki uwanjani na uliimwengu mzima lakini, yalikodolewa mshindi wa mita 800 wanawake-muafrika kusini Caster Semenya aletoroka na medali ya dhahabu akmpku bingwa wa duniia -mkenya Janet Jepkosgei: Wanauliza je, ni mwanamke au ni mwanamume ? Shriikiisho la riadha ulimwenguni (IAAF) limeamua kumchungua.Magazeti ya leo ya nyumbani Afrika Kusini, yamemtangaza Caster Semenya mwenye umbo na misuli ya kiume, "Msichana wa dhahabu"-golden girl.

Kurasa za mbele za magazeti ya Afriika kusini, zimejaa picha zake kwa ushindi wake wa muda wa dakika 1.55.45-muda bora kabisa duniani mwaka huu masafa ya mita 800.Lakini mara tu shirikisho la radha uliimwenguni kutangaza lnamchunguza iiwapo kwel ni mwanamke, baba yake Jacob Semenya alinukuliwa kusema hivi:

"Ni mwanangu wakike.Nimemlea na sijawahi kutiia shaka kuwa si mwanamke.Yeye ni mwanamke na nnaweza kukaririi hayo mara milioni 1."-alisema baba wa bingwa mpya wa dunia wa mita 800.Mkuu wa zaman wa shule aliosoma Semanya,amelambia gazeti la Afrikaans (BEELD) kwamba, Semenya akipenda kucheza na watoto wakiume na hasa dimba na akipenda kuvaa suruali ndefu akienda shule.

Mara moja kwa jiinsi akikerwa na wenzake,maspema mwaka huu kuna watu walotaka asngiie choo cha wanawake: Jibu lake la hasra: "Je mnataka nivue chupi yangu iil muone?Kwa sasa , hadi uchunguzi wa IAAF umetoa jiibu,muafrika kusiini Caster Semanya na sio mkenya Janeth Jepkosgei ndie bingwa wa dunia.

Kenya ilipoteza medali nyengine ya dhahabu katka mbio za mita 1500 wanaume:Medali ya dhahabu iilinyakuliwa na mmzaliwa wa Kenya anaekimbia chiini ya bendera ya Bahrein,Yusuf Kamel na ile ya shaba ametoroka nayo bingwa wa dunia wa mbio hizo,mzaliwa wa Kenya anaekmba kwa Marekani Bernard Lagat.

Shangwe na shamra shamra zilirudi tena katika uwanja wa olimpik wa Berlin kwa usiku wapli baada ya Robert Harting, kuvurumsha kisahani cha chuma-discus- mita 69.43 na kuipatia Ujerumani medalii yake ya pili ya dhahabu .

Baadae alisema:

"Unarusha kisahani ukibahatisha 50-50% mambo yataenda sawa.Kocha wangu akanipa turufu ya mwisho kucheza.Nikavurumisha kisahani kama mzinga na nikashinda." Robert Harting, mwana wa Berlin.

Mwandishi:Ramadhan Ali /AFPE

Mhariri:M.Abdul-Rahman