1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshindi wa Nobel ashindwa Kenya

18 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CIlt

NAIROBI:

Mshindi wa Kenya wa Tuzo la Nobel Bibi Wangari Mathai pamoja na waziri wa zamani wa usalama wameshindwa kuteuliwa na chama chgao kugombea viti vya bunge katika uteuzi uliogubikwa n a machafuko n a mtafaruku-vyombo vya habari vya Kenya vimearifu leo.

Bibi Maathai alietunzwa zawadi ya Nobel mwaka 2004 kwa kutetea usafi wa mazingira,alitorokea chama kidogo baada ya kushindwa na mpinzani wake atakegombea kwa niaba ya chama cha rais Mwai Kibaki PNU huko Tetu,eneo la kati ya Kenya.

Miongoni mwa majina mashuhuri yalioshindwa kuteuliwa na chama cha PNU hapo ijumaa ili kugombea uchaguzi wa Desemba 27 ni pamoja na waziri wa zamani wa usalama wa ndani Chris Murungaru.