1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa wa mauaji ya Rwanda akamatwa

9 Julai 2008

-

https://p.dw.com/p/EYup

FRANKFURT

Mshukiwa wa uhalifu wa kivita nchini Rwanda na ambaye ni mfanyikazi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Callixte Mbarushimana amekamatwa na polisi wa Ujerumani mjini Frankfurt. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na mshtaki wa serikali katika mahakama ya rufaa mjini Frankfurt mtuhumiwa huyo anayetafutwa kwa madai ya kuhusika na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 nchini Rwanda alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Frankfurt akijaribu kusafiri kwenda Saint Petersburg.Serikali ya Rwanda imekuwa ikitaka mtuhumiwa huyo kiongozi wa kundi la waasi wakihutu la FDLR arudishwe nchini humo.Rwanda inamtuhumu Mbarushimana mwenye umri wa miaka 44 kwa mauaji ya kiasi cha watu 30 wa kabila la watutsi wakiwemo waliokuwa wafanyikazi wenzake katika shirika la mpango wa misaada ya maendeleo la UNDP nchini humo.