1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msitu wa Mau Kenya-Kamati yazinduliwa

4 Septemba 2009

Kamati hiyo itasimamia mikakati ya kuhifadhi msitu wa mau

https://p.dw.com/p/JSWR
Mshindi wa tuzo la amani la nobel mwaka 2007, professor Wangari MaathaiPicha: AP

Nchini Kenya, hii leo waziri mkuu Raila Odinga amezindua kamati itakayosimamia mikakati ya kuhifadhi msitu wa Mau. Msitu huo ambao ni chimbuko la mito mingi sio tu nchini Kenya bali pia Afrika mashariki umeharibiwa kiasi cha kuifanya baadhi ya mito hiyo kukauka. Hatima ya maelfu ya watu walioko katika msitu huo itajulikana wiki ijayo baada ya kamati hiyo kuanza kazi yake. Hivi punde nimezungumza na mshindi wa tuzo la amani la Nobel mwaka 2007, Professor Wangari Maathai, na kwanza nilitaka kujua iwapo anahisi kamati iliyozinduliwa leo ina umuhimu wowote

Mwandishi:Jane Nyingi

Mahojiano:Prof Wangari Maathai

Mhariri:Othman Miraji