1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtu mmoja auwawa kaskazini mwa Lebanon

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTz4

Mtu mmoja ameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa kaskazini mwa Lebanon kwenye machafuko kati ya kundi la kiislamu na wafuasi wa mbunge wa Lebanon anayeipinga Syria, Saad Hariri.

Wafuasi wa kundi la Islamic Tawheed na kundi la Tripoli Brigades, wamekabiliana katika kitongoji cha Abi Samra karibu na bandari ya Tripoli.

Mtu aliyeuwawa ni mwanachama wa kundi la Tawheed. Wanajeshi wa Lebanon wametumwa katika eneo hilo kuingilia kati kuyazima machafuko hayo.

Wakati haya yakiarifiwa, shehe mkuu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon, Mohammed Hussein Fadlallah, ametoa fatwa akisema mwanamke muislamu ana haki ya kupigana na mumewe ili kujilinda iwapo atapigwa na mumewe.

Akiitoa fatwa hiyo katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuangamiza mateso dhidi ya wanawake, Fadlallah amesema ingawa dini ya kiislamu inampa mume mamlaka juu ya mwanamke katika kuendesha maswala ya nyumbani, haihalalishi mwanamume atumie nguvu dhidi ya mwanamke pamoja na matusi na maneno ya ukali.