1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtunisha misuli wa kike atupwa jela Iran

Mohammed Khelef
18 Januari 2017

Mtunisha misuli mmoja wa kike amekamatwa nchini Iran, baada ya kutuma picha zinazoonesha sehemu za mwili wake kwenye mitandao ya kijamii, akituhumiwa kwenda kinyume na taratibu za mavazi katika taifa hilo la Kiislamu.

https://p.dw.com/p/2VyFT
Iran Bodybuilderin Shirin Nobahari
Picha: asriran.com

Shirika la habari za kimahakama la nchi hiyo, Mizanonline, limeripoti hivi (Jumatano, 18 Januari) kwamba mtunisha misuli huyo wa kike alikuwa ametuma kile lilichokiita "picha za uchi" mitandaoni. 

Nchini Iran, "uchi" wa mwanamke unamaanisha pia kichwa kisichofunikwa hijab au mikono na miguu ambayo inapaswa kufunikwa awapo kwenye hadhara ya watu.

Mtunisha misuli huyo amepelekwa gerezani kwa kuwa alishindwa kulipa dhamana ya raile milioni mbili (sawa na dola 50,000 za Kimarekani au euro 47,000). 

Ingawa shirika hilo la habari halikumtaja kwa jina mwanamke huyo, inakisiwa kuwa ni mmoja kati ya watunisha misuli wawili wa kike walioshiriki mashindano ya kimataifa.

Wanawake wa Iran wanaruhusiwa kushiriki takribani michezo yote ya kimataifa, ila ni lazima waheshimu utaratibu wa Kiislamu kwenye mavazi yao muda wote.

Mwandishi: Mohammed Khelef/AFP
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman