1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muasisi wa mapambano ya wapalestina afariki.

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyDU

Amman. George Habash, muasisi wa chama chenye msimamo mkali katika mamlaka ya Palestina cha Popular Front for the Liberation of Palestine, PFLP, amefariki dunia nchini Jordan akiwa na umri wa miaka 81. Habash alipata umaarufu akiwa kiongozi wa harakati za kizalendo za Waarabu mwaka 1952 na kuwa mpinzani mkubwa wa mazungumzo ya amani na Israel.

Habash aliasisi chama cha PFLP mwaka 1968 na kujiuzulu kama kiongozi wa chama hicho Julai mwaka 2000. Chama cha PFLP chini ya uongozi wa George Habash kiliteka nyara ndege kwenda Jordan na alitoa wito wa kuangushwa kwa mfalme wa Jordan mwaka 1970 kabla ya mapambano ya kundi la Black September ambapo jeshi la Jordan lilikifukuza chama cha PLO kutoka katika ufalme huo. Habash alizaliwa mwaka 1926 katika mji wa Lydda nchini Palestina , akiwa mtoto wa mfanyabiashara wa Kigiriki muumini wa madhehebu ya Orthodox.