1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muda unayoyoma Marekani

31 Julai 2011

Rais wa Marekani Barack Obama anakutana na wanachama wakuu wa chama cha Demoratic kushughulikia pendekezo jipya, katika jitihada za kufikia maafikiano na kuepusha janga la kushindwa kulipa deni la nchi hiyo

https://p.dw.com/p/126rv
Rais Barack Obama wa MarekaniPicha: AP

Wanachama wa republican pia wanasema wamo katika mazungumzo muhimu na wana imani ya kufikia makubaliano. Mabaraza yote ya wawakilishi na seneti ambayo yanaongozwa na vyama hasimu, yamepinga mapendekezo yaliyowasilishwa. Rais Obama anaetaka kuumaliza mjadala huo wa deni la nchi hiyo, hapo jana, alisisitiza mwito wake kwa pande zote kuafikiana.

Treffen Obama mit Republikanern zu Schuldengesprächen Juli 2011
Rais Barack Obama akikutana na spika wa bunge John Boehner, kushotoPicha: picture alliance/dpa

Marekani ina mpaka saa sita usiku Jumanne, kufikia makubaliano ya kupandisha kiwango cha deni la nchi hiyo, la sivyo itashindwa kulipa madeni yake, hali itakayoweza kuathiri vibaya uchumi duniani.

Mwandishi: Maryam Abdalla/afp rtr cnn dwtv
Mhariri:Martin, Prema