1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muhammad Ali atibiwa homa ya mapafu

22 Desemba 2014

Bondia nguli na bingwa mara tatu wa uzani wa heavyweight Muhammad Ali anaendelea kupata nafuu hospitalini kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu

https://p.dw.com/p/1E8fE
Bildergalerie 40. Jahrestag des Boxkampfes zwischen Ali und Foreman
Picha: AFP/Getty Images

Ali mwenye umri wa miaka 72, anaugua maradhi ya kiharusi, na msemaji wake Bob Gunnell amesema hali yake iko imara tangu alipolazwa katika hospitali moja nchini Marekani siku ya Jumamosi.

Ali aligunduliwa kuwa na kiharusi mnamo mwaka 1984, ikiwa ni miaka mitatu baada ya kustaafu kutoka ulingo wa masumbwi. Bondia huyo wa zamani alionekana hadharani mara ya mwisho mwezi Septemba katika mji wake wa nyumbani wa Louisville, kuhudhuria hafla ya utoaji wa tuzo za kibinaadamu za Muhammad Ali, lakini hakuzungumza.

Mwandishi. Bruce Amani/dpa
Mhariri. Gakuba Daniel