1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNIC:Bomu ndani ya ndege ya abiria?

13 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1e

Ndege ya abiria iliyokuwa na watu 100 ililazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Munic kutokana na tishio la kuwamo bomu ndani ya ndege hiyo.

Ndege hiyo ilikuwa inatoka Paris ikielekea Athens. Polisi ya mji wa Munic iliyotoa habari hizo leo imesema hamkuwa na bomu ndani ya ndege hiyo na wala hakuna habari juu ya nani alietoa vitisho hivyo.