1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH: Benazir Bhutto anataka kugombea uchaguzi

15 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBrg

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto anatazamia kurejea nyumbani baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka minane.Katika mahojiano yake na gazeti la Kijerumani la „Süddeutschen Zeitung“ Bibi Bhutto alisema,anataka kujiandikisha kugombea uchaguzi uliopangwa kufanywa mwishoni mwa mwaka,nchini Pakistan.Benazir Bhutto mwenye umri wa miaka 53 alikuwa mwanamke wa kwanza kushika uongozi wa nchi hiyo ya Kiislamu.Serikali yake ikashindwa kwa sababu ya lawama za rushwa. Rais Pervez Musharraf alieshika madaraka miaka minane iliyopita kwa njia ya mapinduzi,hivi sasa anashinikizwa vikali na umma.Upinzani mkubwa umeundwa dhidi ya kiongozi huyo,baada ya kumfukuza jaji mkuu.Musharraf anataka achaguliwe tena na bunge wakati wa majira ya mapukutiko kwa kipindi kingine cha miaka mitano,kabla ya kufanywa uchaguzi wa bunge jipya.