1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH : Larijani kuhudhuria mkutano wa usalama

10 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTa

Msuluhishi mkuu wa masuala ya nuklea wa Iran atahudhuria mkutano wa usalama wa ngazi juu mjini Munich Ujerumani mwishoni mwa juma hili.

Hapo jana ilielezwa kwamba Ali Larijani hatohudhuria mkutano huo kutokana na kuuguwa lakini waandalizi wa mkutano huo wa Kimataifa wa Usalama wamesema Larijani sasa atahudhuria mkutano huo unaoanza leo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir na mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Havier Solana wanatazamiwa kuwa na mazungumzo yasio rasmi na Larijani kuhusu mpango tata wa nuklea wa Iran.Hii itakuwa mara ya kwanza mjumbe huyo wa Iran kukutana na maafisa wa mataifa ya magharibi tokea Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo nchi hiyo hapo mwezi wa Desemba.

Kutokana na vikwazo hivyo Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomu limekata takriban kwa nusu miradi yake ya misaada ya kiufundi kwa Iran.