1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Munich, Ujerumani. Uturuki haipaswi kujiunga na UA.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2i

Kiongozi wa chama cha kihafidhina cha Christian Social Union nchini Ujerumani kimesema kwa mara nyingine kuwa mazungumzo ya kuiingiza Uturuki katika umoja wa Ulaya ni lazima yasimamishwe.

Edmund Stoiber amewaambia wajumbe wa chama hicho katika mkutano mjini Augsburg kuwa Uturuki haipaswi kuruhusiwa kujiunga na kundi hilo hadi pale itakapoitambua rasmi Cyprus.

Katika masuala ya kidemokrasia , Stoiber amemshutumu kiongozi wa chama cha SPD , Kurt Beck, kwa kutoonyesha mshikamano zaidi na kansela Angela Merkel.

Stoiber amesema chama cha Social Democrats , ambacho kinaunda serikali ya mseto pamoja na chama cha kansela Merkel cha Christian Democrats, kinazuwia miradi muhimu ya mageuzi.