1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Munterfering an’gatuka siasa

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQGO

Naibu Kansela wa Ujerumani anayeondoka madarakani Franz Munterfering ametowa wito kwa serikali ya mseto nchini kushirikiana kwa karibu zaidi.

Munterfering amesema ushirikiano wa vyama hivyo viwili vikuu vya kisiasa nchini cha Social Demnokratik na Christian Demokratik umechangia kuwepo kwa utamaduni wa kisiasa nchini Ujerumani.

Rais Horst Köhler amemuapisha Olaf Scholz kushika wadhifa wa Muntefering wa waziri wa kazi wakati waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank Walter Steinmeir anachukuwa wadhifa wa naibu kansela.

Rais Köhler alimuaga rasmi Munterfering hapo jana mjini Berlin ambapo amemshukuru kwa mchango wa huduma aliotowa kwa wananchi wa Ujerumani na kumpongeza kwa hilo pamoja na kusema kwamba atakuwa anamkosa sana.

Franz Munterfering alijiuzulu kutoka serikalini hapo Novemba 13 ili kupata muda zaidi wa kumshughulikia mke wake ambaye ni mgonjwa.