1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Murray aisaidia Uingereza kushinda Davis Cup

Admin.WagnerD30 Novemba 2015

Andy Murray ameisaidia timu ya taifa ya tennis ya Uingereza kunyakua kwa mara ya kwanza katika historia kombe la Davis la mchezo wa tennis mwishoni mwa juma baada ya kusubiri kwa muda wa miaka 77.

https://p.dw.com/p/1HEtH
Andy Murray Davis Cup Sieg
Picha: Getty Images/LTA/J. Mansfield

Ushindi wa michezo 3-1 dhidi ya Ubelgiji unalipa taifa hilo taji lake la kumi la mchezo huo duniani na unamuweka Murray kuwa shujaa wa tennis baada ya kushinda medali ya dhahabu katika olimpiki mjini London mwaka 2012 na kunyakua ushindi wa kwanza wa ubingwa wa Wimbledon mwaka 2013 na kumaliza miaka 77 ya kusubiri kwa Uingereza. "Ningependa kujifunza mambo machache kutokana na kile kilichotokea mwishoni mwa juma," amesema Murray , ambaye amepata ushindi wa seti 3-0 dhidi ya David Goffin wa Ubelgiji jana na kunyakua ubingwa wa kombe la Davis kwa Uingereza.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae /afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman