1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni aapishwa kwa muhula wa sita madarakani

12 Mei 2021

Rais wa Uganda Yoweri Museveni tayari ameapishwa kwa muhula mwingine wa miaka 5 baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Januari 14 ambao upande wa upinzani ulikataa matokeo yake.

https://p.dw.com/p/3tHjk
Uganda Präsident Yoweri Museveni
Picha: picture-alliance/dpa/I. Langsdon

Halfa ya kuapishwa kwa Museveni ambaye ameitawala Uganda kwa zaidi ya miaka 35 imefanyika mjini Kampala na kuhudhuriwa na zaidi ya wakuu wa nchi 11 wengi kutoka barani Afrika. Marais waliohudhuria ni pamoja na Samia Suluhu waTanzania, Evariste Ndayishimiye wa Burundi, Felix Tshisekedi wa DRC, Salva Kiir wa Sudan Kusini na Mohamed Farmaajo wa Somalia.

Wengine ni Hage Geingob wa Namibia, Sahle Zewde wa Ethiopia, Alpha Conde wa Guinea, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe, pamoja na Nana Akufo-Addo kutoka Ghana

Duru kutoka nchini Uganda zinasema kulikuwa na ulinzi mkali wa jeshi na polisi saa chache kabla ya kuanza kwa hafla hiyo na kuna ripoti kuwa wanajeshi walizingiza nyumba za wanasiasa wa upinzani akiwemo Robert Kyagulanyi aliyechuana vikali na Museveni kwenye uchaguzi wa Januari.

Museveni mwenye umri wa miaka 76 alichukua madaraka mwaka 1986 kutoka msituni ni moja ya viongozi waliosalia madarakani kwa muda mrefu baranai Afirka na anakosololewa kwa kuongoza Uganda kwa mkono wa chuma.