1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Museveni akaidi miito iliyomtaka afute sheria dhidi ya LGBTQ

1 Juni 2023

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekaidi miito ya kimataifa inayomtaka kufuta sheria dhidi ya ushoga aliyoitia saini, ikihusisha adhabu ya kifo kwa kilichoitwa ''vitendo vilivyokithiri vya ushoga.''

https://p.dw.com/p/4S39e
Yoweri Musevini to sign anti-LGBT law
Picha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Akizungumza katika mkutano wa maafisa wa chama chake cha NRM Museveni amesema sheria imesainiwa, na hakuna anayeweza kubadilisha mawazo yao.

Amesema kamwe chama chake hakitoi kauli tata,  na kwamba kinalolisema mchana ni hilo hilo kitalirudia usiku. Wanaharakati nchini Uganda wamewataka wahisani wa kimataifa kuwawekea vikwazo viongozi wa Uganda, kwa sababu ya  sheria hiyo inayochukuliwa kuwa miongoni mwa zile kali sana duniani dhidi ya ushoga.

Tangazo la pamoja la mashirika ya kutetea haki za binadamu limeilaani sheria hiyo, likiitaja kuwa ya hatari na ya kibaguzi.