1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni amuapisha spika wa bunge

Admin.WagnerD19 Mei 2016

Rebecca Kadaga ambaye alikuwa spika wa bunge lililopita alichaguliwa tena bila kupingwa na akaapishwa na rais Yoweri Museveni.

https://p.dw.com/p/1Iqkk
Uganda Präsident Yoweri Museveni in Kampala
Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta MuseveniPicha: Reuters/E. Echwalu

Bunge la kumi nchini Uganda limefanya kikao cha kwanza ambapo wamemchagua tena mwanamke kuwa spika huku Jacob Oulanya aliyependekezwa na rais Museveni akishinda katika uchaguzi uliofanyika katika mazingira ya joto kali la kisiasa. Kulingana na baadhi ya wabunge waliokuwa wakimuunga mkono Muhamad Nserreko aliyepinga ushauri wa rais Museveni kutosimama kwenye mkutano wa wabunge wa chama hicho wiki iliyopita.