1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni aongoza katika matokeo ya muda

Thelma Mwadzaya19 Februari 2011

Matokeo ya muda ya uchaguzi wa Uganda yanaashiria kuwa Rais aliye madarakani,Yoweri Kaguta Museveni,anaongoza na amepata asilimia 71 ya kura zote milioni 3.5 zilizohesabiwa mpaka sasa.

https://p.dw.com/p/10KWm
Rais Museveni wa UgandaPicha: DW/Schlindwein

Kulingana na Tume ya Uchaguzi ya Uganda,Rais Museveni anaongoza na mpinzani wake mkuu amepata asilimia 22.9 ya kura zilizohesabiwa mpaka sasa.

Wahlen Uganda Flash-Galerie
Foleni za wapiga kura mjini KampalaPicha: AP

Hata hivyo tume hiyo haijatoa idadi kamili ya watu waliopiga kura ila inaaminika kuwa imeipita asilimia 69 iliyokuwako katika uchaguzi wa rais uliopita wa mwaka 2006.Matokeo kamili yatatangazwa rasmi hapo kesho.