1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf amuhakikishia Brown kuondoa hali ya hatari

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CS1A

Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown amesema,Rais wa Pakistan Pervez Musharraf amemuhakikishia kuwa ataondosha hali ya hatari na atajiuzulu kama mkuu wa majeshi.Brown,alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini London kabla ya kuelekea Kampala,nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola.

Kwa upande mwingine,Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza David Miliband amesema,Jumuiya ya Madola na hata jumuiya ya kimataifa kwa jumla, zinakubaliana kuwa Musharraf anapaswa kujiuzulu kama mkuu wa majeshi na kurejesha utawala wa kisheria.

Mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola utaamua kama Pakistan isimamishiwe uanachama wake katika jumuiya hiyo,iwapo Musharraf hatoondosha hali ya hatari na kujiuzulu kama mkuu wa majeshi.