1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf atakiwa kuondowa hali ya hatari

Mohamed Dahman17 Novemba 2007

Mjumbe mwandamizi wa Marekani amekutana na Rais Pervez Musharraf wa Pakistan na washauri wake wa karibu leo hii kuwasilisha ujumbe mkali sana wa kuondolewa kwa utawala wa hali ya hatari nchini humo

https://p.dw.com/p/CImb
John Negraponte naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani.
John Negraponte naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani.Picha: AP

John Negraponte naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani wamejadili na Musharraf mzozo wa kisiasa nchini humo na hali nzima ya eneo hilo kutokana na machafuko yanayosababishwa na kundi la Al Qaeda na Taliban.

Wanadiplomasia wa mataifa ya magharibi wanasema Negraponte atamtaka Musharraf kuondowa utawala wa hali ya hatari mara moja,kujiuzulu wadhifa wa ukuu wa majeshi, kuitisha uchaguzi,kuondowa vikwazo dhidi ya vyombo vya habari na kuwaachilia wafungwa wa kisiasa.