1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf kuitisha uchaguzi Februari

P.Martin9 Novemba 2007

Rais wa Pakistan,Jemadari Pervez Musharraf anasema,uchaguzi mkuu wa bunge utafanywa kabla ya kati kati ya mwezi Februari.

https://p.dw.com/p/C774
Wanasheria wakiandamana mjini Peshawar kupinga amri ya hali ya hatari nchini Pakistan
Wanasheria wakiandamana mjini Peshawar kupinga amri ya hali ya hatari nchini PakistanPicha: AP

Musharraf,tangu kutangaza hali ya hatari Jumamosi iliyopita, anashinikizwa na washirika wake wa magharibi na wanasiasa wa upinzani kuufanya uchaguzi mwezi wa Januari kama ilivyopangwa hapo awali.

Kwa upande mwingine,waandamanaji wamemiminika tena mitaani,bila ya kujali amri inayopiga marufuku mikutano ya hadharani.Upande wa upinzani umesema,mamia ya wafuasi wake walikamatwa usiku uliopita katika juhudi ya kuwazuia kushiriki katika maandamano makubwa ya kupinga amri ya hali ya hatari.

Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan,Benazir Bhutto alie kiongozi wa chama cha upinzani cha PPP, amewahimiza wafuasi wake kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanywaa leo Ijumaa mjini Rawalpindi.