1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf yuko Ufaransa

22 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cw6o

PARIS:

Rais wa Pakistan Perves Musharraf ameanza mazungumzo yake na mwenyeji wake Ufaransa ,Nicolas Sarkozy mjini Paris. Ufaransa ikikariri nchi za Marekani, na Umoja wa Ulaya , nayo imemhimiza Mushrraf kuhakikisha kuwa uchaguzi ujao unakuwa huru na wa haki.

Ziara ya Bw Musharraf njini Paris ndio kituo cha pili cha safari yake katika bara la Ulaya. Aidha atahudhuria mkutano wa kiuchumi wa Davos na baadae kuelekea nchini Uingereza. Kituo chake cha kwanza cha safari yake hii kilikuwa Brussels( Brasols) ambako alikutana na mratibu wa masuala ya kigeni ya Umoja wa Ulaya-Javier( Havia) Solana pamoja na katibu mkuu wa NATO Jaap( Yap) de Hoop Scheffer.Musharraf ameuambia Umoja wa Ulaya kuipa mda nchi yake kuweza kurekebisha mambo.

Kuhusu masuala ya usalama,Musharraf ameungwa mkono na Scheffer,ambae alisema kiongozi huyo wa Pakistan ni sehemu ya ufumbuzi wa usalama na wala sio tatizo.