1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa kilimo wa Malawi afutwa kazi kwa ufisadi

Isaac Gamba
22 Februari 2017

Rais Peter Mutharika wa Malawi amemfukuza kazi waziri wake wa kilimo kufuatia uchunguzi uliofanyika juu ya ufisadi kwenye manunuzi ya mahindi katika wakati taifa hilo likikabiliwa na njaa.

https://p.dw.com/p/2Y2Kg
Peter Mutharika wird neuer Präsident von Malawi 31.05.2014
Picha: AFP/Getty Images

George Chaponda ameondoshwa kwenye wadhifa wake kwa kubainika kuzidisha gharama za manunuzi ya mahindi kutoka Zambia.

Jumla ya dola milioni 34.5 zimetumika na taifa hilo la kusini mwa Afrika, ambalo linakabiliwa na kitisho cha njaa kama yalivyo maeneo kadhaa ya eneo hilo, lakini imefahamika kuwa mamilioni ya fedha hizo yalihifadhiwa nyumbani kwa Chaponda.

"Rais amemuondoa Chaponda kama waziri wa kilimo mara moja baada ya kugundulika akiwa na mamilioni ya fedha nyumbani kwake jana," Waziri wa Habari Nicolaus Saudi ameliambia shirika la habari la Reuters leo (22 Februari).

Mwezi uliopita, Rais Mutharika alikuwa ameagiza uliopita uchunguzi kuhusina na manunuzi hayo.