1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano mpya wa kibalozi wazuka kati ya Uingereza na Urusi

15 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CphM

MOSCOW:

Urusi imekasirishwa na hatua ya Uingereza ya kufungua tena ofisi za shirika la kiutamaduni la Uingereza la British Council mjini Moscow licha ya agizo la awali la kufunga ofisi mbili za shirika hilo .

Serikali ya Urusi imesema hatua hii ni uchokozi wa kimakusudi na kuahidi kuchukua hatua kali mkiwemo kuwanyima Visa wafanya kazi wa shirika hilo.Uingereza ilikataa agizo hilo siku ya jumatatu.Balozi wa Uingereza mjini Moscow- Antony Brenton amesema kuwa afisi za British Council zitabaki wazi na hatua yoyote dhidi ya shirika hilo itakuwa inavunja sheria za kimataifa. Asema uamuzi wa kufungua ofisi zao ni baada ya mapumziko ya majira ya baridi.na anaamini kuwa wanafuata sheria ya mwaka wa 1994 ya mkataba wa kiutamaduni kati ya Uingereza na Urusi. Aidhaa anaamini kuwa wanafanya kazi katika mazingira ya sheria za Urusi.

Mwezi jana serikali ya Urusi iliamuru ofisi hizo zifungwe ikisema zinaendesha kazi zake kinyume na sheria.Hatua ya sasa ni maendeleo ya msururu wa mvutano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulioanza baada ya mtoro wa Kirusi Alexander Litvinenko kupewa sumu mjini London mwaka wa 2006.Maofisa wa ubalozi wa pande zote mbili walifukuzwa katika kipindi cha kiangazi baada ya Moscow kukataa kumkabidhi jasusi wa zamani wa KGB Andrei Lugovoi,anaetakiwa Uingereza kwa madai ya kumuua Litvinenko.