1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano wa kisiasa watokota nchini Iran

27 Julai 2009

Rais Mahmoud AhmedNejad awatimua mawaziri wake

https://p.dw.com/p/IyHd
Rais Mahmoud Ahmadinejad, Esfandiar Rahim Mashai, aliyetimuliwa kuwa makamu wa rais baada ya malalamiko ndani ya serikali.''Picha: AP

Nchini Iran mzozo wa kisiasa unatokota, huku arais mahmoud Ahmadinejad akikosolewa kwa kumfukuza kazi waziri wake wa usalama, ukiwa ni mgogoro mpya tangu nchi hiyo kukumbwa na wimbi la maandamano ya upinzani baada ya uchaguzi wa rais mwezi uliopita.

Rais Ahmadinejad anayetarajiwa kuapishwa bungeni na kulitangaza baraza lake la mawaziri mwezi ujao, pia alishuhudia waziri wake wa utamaduni akijiuzulu kutokana na kile alichokiita kuwa ni "Serikali dhaifu."

Lakini shirika la habari MEHR liinukuu duru moja rasmi ikisema kwamba waziri huyo Gholam Hussein Mohseni Ejeie alifukuzwa baada ya kubishana na rais Ahmedinejad katika mkutano wa baraza la mawaziri kutokana na uteuzi wake wa makamu wa rais uliozusha malalamiko.

Hatimae Esfandiar Rahim Mashaie alijiuzulu kama makamu wa kwanza wa rais, pale kiongozi mkuu na mwenye usemi wa mwisho ayatollah Khamenei alipoingilia kati na kumuamuru Ahmedinejad amfukuze kazi.

Kwa upande wake Mashaie aliwakasirisha wale wenye msimamo mkali mwaka jana, aliposema Iran ni rafiki wa watu wa Israel. gazeti la Khabar lilikua na kichwa cha maneno" Kufukuzwa - ni matokeo ya kumpinga Ahmedinejad."

Kabla hajakaa sawa rais huyo wa Iran alipata pigo jengine baada ya waziri wa utamaduni Mohammad Hossein Safaar Harandi naye kujiuzulu na barua yake kuchapishwa shirika la habari la FARS jana.Matukio hayo yameitumbukiza serikali ya rais Ahmedinejad katika hali ya wasiwasi na mvutano kama anavyosema mchambuzi wa masuala ya kisiasa Amir Mousawi kutoka Teheran-

''Hapa Kuna suala muhimu sana juu ya kujiuzulu mawaziri hawa.kwamujibu wa Ali Mutahat kiongozi wa kundi la kihafidhina ambalo ndo kubwa bungeni alisema kwamba serikali ya Ahmedinejad imepoteza uhalali wake kwa mujibu wa katiba kwasababu baada ya kujiuzulu mawaziri 4 inamaanisha mawaziri 15 wamejiuzulu kutoka serikali yake tangu alipokamata madaraka ya urais kwenye awamu ya kwanza miaka 4 iliyopita.Na kwamujibu wa katiba nusu ya mawaziri wakijuzulu inabidi rais apate idhini ya pili kutoka bungeni kwahivyo rais AhmedNejad anakabiliana na mtihani mgumu katika siku zake hizi za mwisho''

Taifa hilo la Uajemi limeingia katika msukosuko wa kisiasa tangu uchaguzi wa rais Juni 12, ambao matokeo yake yalizusha maandamano na ghasia kupinga uamuzi wa tume ya uchaguzi kumtangaza Ahmedinejad kuwa mshindi.

Iran 17_07_2009
''Ghasia za uchaguzi zimeibua mgawanyiko ndani ya uongozi wa Iran''Picha: AP

Machafuko hayo baada ya uchaguzi ambayo ni mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu mapinduzi ya Kiislamu 1979, pia yameibua mivutano miongoni mwa watawala na kuzusha lawama kali sio tu dhidi ya Ahmedinejad bali pia kiongozi mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

Kinachosubiriwa hivi sasa ni iwapo baraza lijalo la mawaziri wa Ahmedinejad litaidhinishwa bila matatizo na bunge. katika kipindi chake cha asasa ameshabadili mawaziri 10 katika baraza lake la mawaziri 21.

Tayari rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani na kiongozi wa kamati inayosimamia masuala makuu ya kisiasa, inayoangalia pia shughuli za kiongozi mkuu Khamenei ameituhumu serikali kuwa tangu matokeo ya uchaguzi inaanza kupoteza imani ya umma, na kutoa wito wa kuachiwa huru mamia ya watu waliokamatwa kutokana na machafuko ya baada ya uchaguzi.

Mwandishi : Ramadhan Yusuf Saumu / AFPE

Mahariri:M.Abdul-Rahman