1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano waendelea kati ya jaji Chaudry na Musharaf nchini Pakistan

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxo

Wakili mashuhuri wa zamani nchini Pakistan amewahutubia maelfu ya wafuasi wake karibu na korti kuu ya mjini Islamabad,akimshambulia bila ya kumtaja kwa jina rais Pervez Musharraf.Mwanasheria mkuu huyo wa zamani,IFTIKHAR CHAUDRY amesema ni muhimu kuendelea kutenganisha madaraka ya kisiasa.Ingawa hakumtaja rais Musharaff kwa jina,IFTIKHAR CHAUDRY amesema ni makosa madaraka yote kukabidhiwa mtu mmoja.Pervez Musharraf sio tuu ni rais bali pia kiongozi wa vikosi vya wanajeshi wa Pakistan.Mkutano aliokua amepanga kuuitisha mjini Karachi uliakhirishwa hivi karibuni baada ya ziara yake kusababisha machafuko yaliyogharimu maidha ya watu 41 mjini humo.Rais Musharaff amemfukuza kazi jaji Chaudry miezi miwili iliyopita.