1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano waendelea kati ya serikali ya Palestina na Umoja wa Ulaya.

11 Aprili 2007

Umoja wa Ulaya umesema hauna nia yeyote kutoa uafadhili wa kifedha kwa serikali ya Palestina hadi serikali hiyo itakapotimiza masharti matatu ya amani.Haya yametokana na takwa la waziri wa fedha wa Palestina Salam Fayyad, aliyeomba msaada wa dolla billioni moja kusaidia serikali yake.

https://p.dw.com/p/CHGV

Waziri wa fedha wa serikali ya ndani ya wapalestina Salam Fayyad baada ya kukutana na kamishna wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Benita Ferrero-Waldner,alisema ufadhili wa dolla billioni moja wanawoutafuta, utasaidia serikali mpya ya kitaifa ya umoja wa Palestina kuendesha shughuli zake mwaka huu wa 2007.

Hata hivyo, Umoja wa Ulaya ulisema kuwa uko tayari tuu kuisaidia serikali hiyo kuhakikisha kuna uwazi wa makadirio ya fedha zake. Kadhalika wataendelea kutoa fedha tuu kwa mashirika ya misaada ya kiutu yanayowasaidia wenyeji wa Palestine.

Umoja wa Ulaya na mataifa mengine ya wafadhili pamoja na Marekani yalisimamisha utoaji wa fedha wa Palestina mwaka jana baada ya chama cha Hamas kuchukua nafasi kubwa katika uongozi serikalini.

Hamas imetajwa kuwa ni kundi la magaidi,na mataifa ya Umoja wa Ulaya na Marekani yalisema kuwapa ufadhili ni sawa na kusaidia mipango ya magaidi. Kamishna wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya, Benita Ferrero-Waldner, alisema wako tayari kufanya kazi na mawaziri wasioshirikiana na kundi la Hamas. Alisistiza pia lazima Palestina itekeleze maazimio matatu ya kudumisha amani na kulitambua taifa la Israel.

Palestine haikabiliwi tuu na matatizo ya kifedha bali pia mzozo wake kuhusu kuachiliwa huru wafungwa wa Kipalestine na Israel. Israel inataka Gilad Shalit, aliyetekwa miezi kumi iliyopita na kundi la Hamas aachiliwe huru. Lakini Palestina nayo imekataa kuwachilia hadi Israel itakapokubali kuwaachilia wafungwa mia nne hamsini wa Kipalestina.

Israel imeripotiwa kuipuuza orodha waliodai ina majina ya wafungwa waliomawaga damu za raia wao, kama vile Marwan Barghuti,na baadhi ya viongozi wakuu wa Hamas. Hatahivyo licha ya tetesi hizo ishara nzuri ni kuwa Israel inataka kuendelea na majadiliano baina yao na Palestine, kupitia wapatanishi wa Misri.

Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, na rais wa Palestine Mahmmoud Abbas wanatarajiwa kukutana siku ya Jumapili katika mkutano wao wa kwanza tangu walipokutana na waziri wa mambo ya nje, Condolezza Rice. Msemaji wa olmert, Miri Eisin, alisema hawajafahamishwa watakutana wapi,lakini wanatarajiwa kuyajadili masuala haya ya mateka na makubalianao ya amani.

Rais Mahmmoud Abbas anatarajia kuwa waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert, atakubali mazungumzo ya amani kwa msingi wa maazimio ya amani ya nchi za kiarabu. Ambapo Israel itashurutishwa kurudisha ardhi walizoziteka mwaka 1967. Lakini duru za Israel na nchi za Magharibi zimesema uamuzi huo utakuwa kizuizi kikubwa kuleta amani baina ya mataifa haya ya Israel na Palestina.

Isabella Mwagodi