1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mvutano wazuka Marekani kutokana na maandamano ya Gaza

Sylvia Mwehozi
23 Aprili 2024

Ghasia zimezuka kati ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina na viongozi wa Vyuo Vikuu kadhaa vya Marekani , huku masomo yakisitishwa na waandamanaji kukamatwa.

https://p.dw.com/p/4f5Tx
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Marekani waandamana
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Marekani waandamanaPicha: Fatih Aktas/AA/picture alliance

Maandamano hayo yaliyoanza wiki iliyopita katika Chuo Kikuu cha Colombia yakihusisha kundi kubwa la waandamanaji walioanzisha kambi ya mshikamano wa Gaza, yameenea hadi kwenye vyuo vikuu vingine.

Baadhi ya wanafunzi wa Kiyahudi katika Chuo Kikuu cha Colombia, wameripoti vitisho na vitendo vya chuki wakati wa maandamano hayo ya siku kadhaa, yanayoshinikiza taasisi za New York kuachana na makampuni yanayounga mkono Israel.

Mamlaka zimelazimika kuhamishia madarasa mtandaoni kufuatia ghasia hizo. Wiki iliyopita zaidi ya waandamanaji 100 walikamatwa baada ya viongozi wa vyuo vikuu kuomba usaidizi wa polisi katika viunga vya vyuo hivyo.