1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwafaka Ireland ya Kaskazini

27 Machi 2007

Mada 2 zimetia leo fora katika safu za wahariri wa magazeti ya Ujerumani-nazo ni mjadala juu ya malipo ya chini kabisa ya mshahara nchini Ujerumani na muafaka wa kuunda serikali ya pamoja huko Ireland ya kaskazini kati ya wakatoliki na waprotestanti.

https://p.dw.com/p/CHTP

Gazeti la BADISCHE TAGBLATT kutoka Baden-Baden laandika ni kinyume na mila na desturi mtu kufanya kazi kimalifu halafu kuona hapati ujira wa jasho lake .Lazima hapo kuna kilichokwenda kombo nchini humu.Mjadala wote kuhusu malipo ya ujira mdogo kabisa unaelekeza katika swali la kimsingi-nalo iwapo Ujerumani inahitaji sheria ya kuhakikisha kiwango cha chini kabisa cha mshahara.Chama cha CDU kinajenga hoja ya kukataa mpango huo.Kinatumia hoja ya uhuru wa kimambo-leo katika soko la kazi.Hoja kama hiyo ya kinadharia ni upuuzi mtupu.

Kwani, nchini Uingereza kuliko na uhuru wa aina hiyo,mbona kuna kima cha chini cha mishahara –lauliza gazeti.

Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG lingependa kujibiwa swali jengine:

Laandika:

“Kabla kupata ufumbuzi wa swali hili,yapasa kujibu sio swali la kinadharia bali hali halisi ya mambo ilivyo; na hasa kwa kutupia jicho mshahara wa mchanganyiko wa kazi mbali mbali-“kombilöhne” ambao unapendekezwa zaidi na CDU badala kima cha chini cha mshahara .Nafasi ngapi za kazi serikali inataka kutoa kwa kila hali ?

Kabla haikupata jibu la swali hili,serikali ya vyama vya muungano ya Ujerumani itabidi kulishughulikia swali la ujira wa chini kabisa lakini bila mwishoe, kupata matokeo ya kuridhisha.”

Kwa jicho la gazeti la WESTFÄLISCHE RUNDSCHAU mkasa huu mzima ni kampeni za uchaguzi.

Laandika:

“Sasa au baadae,vyama vya SPD na CDU/CSU vitatengana katika serikali yao ya muungano .Hapo tena ni dhahiri shahiri,vitazibainisha wazi tofauti zao juu ya mada hii.

Kukosoa mabishano kama hayo si siasa. Demokrasia inaingiza mabishano ya fikra.Yastaajabisha laki,kukiona chama cha SPD kimeanza kampeni ya uchaguzi hata bado kutangazwa imeaanza na kinakusanya saini za kuungamkono mpango wa kuwapo malipo ya chini kabisa ya mshahara.Vyama vya CDU/CSU hapo vitajikuta vimebanwa.Na huo si mtindo mzuri kufanyiana washirika serikalini-laandika Westfälische Rundschau.

Likitugeuzia mada,gazeti la Stuttgarter Zeitung lazungumzia muafaka uliofikiwa na wafuasi wa madhehebu mbili za Ireland ya kaskazini-waprotestanti na wakatoliki.Kwa jicho la gazeti hilo muafaka huo unatoa matumaini kwavile Kiongozi wa chama cha DUP Ian Paisley,anaungwamkono na chama chake.

Gazeti laandika:

“sasa Ian Paisley amejiendea kinyume mwenyewe kwa kuridhia kuunda serikali pamoja na chama cha Sinn Fein.Hatahivyo, ni hiyana njema alioifanya.Aliiandaa kwa matamshi makali na kupitia uchaguzi wa wiki 3 nyuma aaliipatia baraka za chama chake cha waprotestanti.

Hali ni sawa na hiyo upande wa kiongozi wa Sinn-Fein-Gerry Adams, ambae ameridhia wanamgambo wake wa IRA kukubali mamlaka ya polisi wa Ireland ya kaskazini na kuwa chini yao.

Wanasiasa wote wawili, wanastahiki sifa kwa kuwa baada ya umwagaji damu wa miaka kadhaa wameweza sasa kufikia muafaka.Ndio maana serikali hii mpya ya pamoja ukilinganisha na ile ya miaka 5 nyuma ,hii yatoa matumaini.”

Gazeti la RHEINPFALZ linalochapishwa Ludwigshafen linasisitiza kuwa, wakatoliki sawa na waprotestanti huko Ireland ya kaskazini, wanakodoa macho kusini mwa jimbo lao kwa uchu:Jamhuri ya Ireland imestawi kiuchumi na ina neema.Na wao sasa waweza kuanza kuifukuzia.Wananchi wa huko wanastahiki neema hiyo.

Kwani, wengi wao wamekuwa wahanga na sio watendaji wa ugomvi na uwamgaji damu kunyan’ganyia mamlaka Ireland ya kaskazini.Endapo elimu na neema itazagaa kwa wote bila kujali madhehebu yao,swali la kuiunganisha tena Ireland

alitakua na uzito tena.