1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mpya 2012 utakuwa wa matatizo; Merkel

Sekione Kitojo1 Januari 2012

Kansela Angela Merkel katika hotuba yake ya kuukaribisha mwaka mpya 2012 amegusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na masuala ya kimataifa na ndani ya nchi.

https://p.dw.com/p/13cPl
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akitoa hotuba yake ya mwaka mpya.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani akitoa hotuba yake ya mwaka mpya.Picha: dapd

Katika hotuba yake kansela alianzia kwa kuangalia masuala ya kimataifa. Amesema kuwa mwanzoni mwa mwaka huu lilianza vuguvugu la mageuzi ya kisiasa katika mataifa ya Afrika kaskazini na mashariki ya kati. Mwezi March Japan ilikumbwa na tetemeko kubwa la ardhi , na kusababisha maafa makubwa ya kinyuklia. na katika majira ya mapukutiko mwishoni mwa mwaka huu mkaazi wa bilioni saba alizaliwa katika jumla ya wakaazi duniani.

epa03035392 (FILE) A file photo dated 12 November 2011 showing a general view of the crippled Fukushima Dai-ichi nuclear power station in Okuma, Fukushima Prefecture, Japan. A cold shutdown has been achieved at a Japanese nuclear plant damaged in an earthquake and tsunami after nine months of efforts to bring the facility under control, the government said 16 December 2011. A cold shutdown means no nuclear reactions are occurring at the Fukushima Daiichi Nuclear Station, 250 kilometres north-east of Tokyo, and little radiation is leaking into the environment, marking an end to the emergency phase of Japan's worst nuclear disaster and the start of the clean-up and scrapping of the reactors. The government said the announcement meant that the goal to achieve a cold shutdown by year's end had been achieved, but environmentalists criticized it as a conscious deception, saying the reactors were far from stable. EPA/David Guttenfelder / POOL *** Local Caption *** 00000403000698 +++(c) dpa - Bildfunk+++
Kinu cha kinuklia cha Fukushima nchini JapanPicha: picture-alliance/dpa

Ameongeza kuwa ulikuwa mwaka wenye mabadiliko makubwa. Hayo pia yalitokea katika bara la Ulaya.

Katika bara la Ulaya hali iliendelea kuwa mbaya ya madeni ya nchi, amesema kansela, na kuongeza kuwa mbali ya matatizo yote hayo hatukusahau, kwamba kuishi kwa usalama ni zawadi ya kihistoria kwa bara hili. Kwa muda wa nusu karne kumekuwa na uhuru , amani , sheria , haki za binadamu na demokrasia.

Maadili haya tusingeweza pia katika enzi hizi kuyalinda vizuri. Kwa hivi sasa , ambapo bara la Ulaya linajikuta katika wakati mgumu kabisa kuwahi kutokea kwa karne kadha, natambua kuwa mnafikiria kuhusu usalama wa sarafu yetu. Amesema kuwa bara la Ulaya linapambana na mzozo huu kwa pamoja , licha ya kuwa njia kuelekea kuudhibiti mzozo huo ni ndefu na itakuwa na matatizo.

Kuhusu hali ya hapa Ujerumani kansela amesema :

Hapa Ujerumani tuna sababu ya kuwa na matumaini. Kwani karibu kila kijana wetu amepata nafasi ya masomo katika mwaka huu. Ni watu wachache wasio na ajira. Ujerumani imo katika njia iliyo sahihi, licha ya kuwa mwakani bila shaka kutakuwa na hali ngumu.

Hiyo ni sehemu ya hotuba ya kansela Angela Merkel ya kuukaribisha mwaka mpya 2012.