1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwalimu apewa msamaha na rais.

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CW2N

Khartoum. Rais Omar al-Bashir wa Sudan ametoa msamaha kamili kwa mwalimu raia wa Uingereza ambaye amehukumiwa kifungo cha siku 15 jela kwa kosa la kukufuru. Rais huyo alitangaza msamaha huo baada ya kukutana na wanasiasa wawili wa Uingereza ambao ni Waislamu ambao wamekwenda nchini Sudan kwa nia ya kupata kuachiliwa kwa mwanamke huyo Gillian Gibbons. Anatarajiwa kurejea nyumbani Uingereza kesho Jumanne.

Gibbons alifungwa jela kwa kuutusi Uislamu kwa kuwaruhusu wanafunzi wake kumpa jina la Mohammed mwanasesere mwenye umri wa dubu anayefahamika zaidi katika nchi za magharibi kama Teddy bear. Watu wenye imani kali ya dini walitaka auwawe licha ya kuwa wengi wa watu wa Sudan wanafikiri kuwa ilikuwa ni makosa tu ya kutofahamu, wakati ambapo kuomba msahama ilikuwa inatosha.