1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwana mfalme William na Kate wamefunga ndoa!

29 Aprili 2011

Ndoa ya kifalme inayofanyika leo nchini Uingrezea inafuatiliwa kwa makini nchini Ujerumani vile vile. Jumuiya moja ya hapa nchini inayoifuatilia ndoa hiyo kwa moyo wote inataka ufalme urudishwe

https://p.dw.com/p/115pf
Mwana mfalme William na mpenzi wake Kate Middleton

Mwenyekiti wa chama jumuiya hiyo inataka kurudishwa a kwa mfumo wa kifalme nchini Ujerumani Knut Wissenbacha amesema, ''Sisi katika chama chetu kinachoitwa Jadi na Maisha tumejipa jkumu la kuunga mkono wazo juu ya kurudishwa tena mfumo wa kifalme nchini Ujerumani na kuudumisha"

Mwenyekiti huyo, Bwana Wissenbach haishi katika kasri bali nyumba ya kawaida katika mji wa Niederheimbach ulioko jimbo la kaskazini mwa Ujerumani. Mpenda ufalme huyo ambaye sasa ana umri wa miaka 40 ni mtumishi wa serikali. Anapitisha wakati wake wa faragha kwa kukusanya picha za wafalme wa kijerumani, nishani na sare za wafalme.

Katika ofisi yake ameweka tandiko la farasi badala ya kiti.

Prinz William Kate Middleton Park Darwen Flash-Galerie
Maharusi: Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa pili na mpenzi wake Kate MiddletonPicha: picture-alliance/dpa

Sare za wafalme

Katika tandiko hilo la farasi aliwahi kukaa mfalme Wilhelm wa pili aliekuwa mfalme wa mwisho hadi mwaka wa 1918 nchini Ujerumani.

Kwa mtazamo wa mwenyekiti wa chama cha wapenda ufalme , Knut Wissenbach mjerumani ambaye angelistahili kuwa mfalme wa Ujerumani ni Prince wa Hohenzolern- Georg Friedrich.

Chama cha Knut Wissenbach kina wanachama 200 wanaoliunga mkono wazo la mwenyekiti wao. Kura ya maoni iliyofanyika hivi karibuni imeonyesha kwamba asilimia 15 ya wajerumani wangelikuwa tayari kuukubali mfumo wa kifalme.

Flash-Galerie Vorbereitungen der Hochzeit von Prinz William und Kate Middleton
Farasi wa kifahari watakaomsindikiza Malkia Elizabeth wa piliPicha: dapd

Madaha na madoido

Watu hao wanataka kuona madaha na madoido ya kifalme katika uongozi badala ya kumwona Rais , ambaye wanasema anachusha.

Lakini hakuna matumaini ya kurejea tena mfumo wa kifalme nchini Ujerumani kama anavyosema mtaalamu wa masuala ya kifalme Bibi Monika Wienfort. ''Naamini kwa jumla kwamba kurudishwa tena mfumo wa kifalme nchini Ujerumani au nchini Austria siyo suala la kuzungumzwa asilani."

Großbritannien London Königin Elizabeth II Thronrede
Malkia Elizabeth wa PiliPicha: AP

Mtaalamu huyo ambaye ni mhadhiri kwenye chuo kikuu cha North Carolina nchini Marekani, amesema mfumo wa kifalme nchini Ujerumani ulifikia mwisho baada ya vita kuu ya pili ya dunia.

Mwandishi: Riegert, Bernd /ZPR/ Mtullya Abdul

Mhariri:Josephat Charo