1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanadiplomasia wa Marekani auwawa

1 Januari 2008

---

https://p.dw.com/p/Cit3

KHARTOUM

Mwanadiplomasia wa Marekani amefariki kutokana na majeraha mabaya aliyoyapata baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi mapema leo hii na dereva wake kuuwawa katika mji mkuu wa Sudan Khartoum.Kwa mujibu wa mfanyikazi mmoja katika ubalozi wa Marekani nchini humo,watu wasiojulikana walifyatulia risasi gari la mwanadiplomasia huyo usiku wa manane katika wilaya ya Al Amrat.Tukio hilo limeripotiwa siku moja baada ya kikosi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa kuchukua jukumu la kuweka amani katika jimbo tete la Darfur.Ubalozi wa Marekani mjini Khartoum umesema haijakuwa wazi ikiwa shambulio hili limechochewa kisiasa au ni uhalifu wa kawaida.